Mama Yetu wa Fatima
"Kwa Yeyote Atakayeizingatia Ibada Hii Naahidi Wokovu"...Mama Yetu wa Fatima, 13 Juni 1917
Ahadi iliyoje, ya ajabu na ya kushangaza iliyotokea siku ya
tarehe 13 Juni 1917! Ingawaje licha ya ahadi hii bado tunashawishika kuwa na
mashaka. Yasinta wa Fatima, kwa neema ya pekee, alihisi moyo wake kujawa na
mapendo makuu kwa Moyo Safi wa Maria. Je, sisi? Tumekuwa wavivu au juhudi yetu
ni ya muda mfupi tu! Je, tungeweza kujua kama tungekuwa na moyo wa ibada wa
kutosha ili Mama Yetu ingembidi kutimiza ahadi Yake kwetu?
Ni hapa ndipo tunashangazwa na Huruma Kuu isiyo na mipaka, na
sifa ambayo zaidi ni ya Kikatoliki ya ufunuo wa Fatima. Katika ujumbe mzima,
hakuna hata tone moja la mawazo ya Kiprotestanti! Hapa, Mbingu imekwenda hadi
kwenye mipaka ya upendeleo, na tabiri kuu kuliko zote ("Mungu anataka
kuthibitisha duniani moyo wa ibada kwa Moyo Wangu usio na doa")
zimebadilishwa, na kutafsiriwa katika maombi madogo kabisa, maombi ya wazi na
halisi, maombi rahisi yasiyokuwa na chembe yoyote ya mashaka. Kila mmoja anaweza
kutambua kama ameyatimiza au la. "Ibada ndogo" ikitekelezwa kwa moyo
wa bidii, hii inatosha kwetu kupata neema - ex opere operato, unaweza kusema, sawa kama ilivyo kwa sakramenti; na neema
iliyoje - neema ya wokovu wa milele! Inastahili kuchunguza kwa makini ahadi hii
kuu. Ni utimizaji, utekelezaji kamili wa sehemu ya kwanza ya Siri kuu ambayo
yote inahusu wokovu wa roho.
Kutoka Fatima hadi Pontevedra:
utimizaji wa Siri.
Katika kusimulia matukio na kuelezea ujumbe wa Pontevedra,
tutazungumzia kwa kifupi maneno yaliyotamkwa na Mama Yetu tarehe 13 Julai 1917.
Ni mafupi, lakini yamejaa maana kubwa sana:
"Kama ninayowaambieni yatatekelezwa, roho nyingi zitaokolewa Â…
Nitafika kuomba Komunio ya Malipizi ya dhambi kila Jumamosi za kwanza za mwezi."
Hii basi ndiyo "Siri ya kwanza ya Maria" ambayo
lazima tuichambue na kuielewa. Ni njia ya uhakika na rahisi ya kuokoa roho
zisipotee motoni; kwanza roho zetu wenyewe, halafu zile za majirani zetu; na
hata roho za wakosefu wakubwa kuliko wote, kwani huruma na nguvu ya Moyo Safi
wa Maria havina mipaka.
Ahadi Kuu ya Jumamosi Tano za Kwanza
Na: Br. Michael wa Utatu Mtakatifu
I. Dibaji
II. Pontevedra: Matukio na
Ujumbe
10 Des. 1925: Tukio la Mtoto Yesu na Mama Yetu
Kujulishwa kwa Ujumbe
Kusubiri kwa mateso
Simulizi ya mwanzounaopendeza
15 Feb. 1926: Tukio jipya la Mtoto Yesu
III. Ahadi Kuu na Masharti Yake 1. Jumamosi
ya Kwanza ya miezi mitano mfululizo
2. Maungamo
3. Komunio ya Malipizi ya Jumamosi za Kwanza
4. Kusali Rozari1
5. Tafakari ya dakika kumi na tano ya Mafumbo Kumi na Tano ya
Rozari
6. Nia ya kufanya Malipizi
IV. Madhumuni ya Ibada ya
Malipizi ya dhambi
Ufunuo wa tarehe 29 Mei 1930
Miiba ya Moyo Safi wa Maria
Kufuru za waasi wa dini, waliofarakana na wanaomdharau Mungu
Kufuru za watoto wakaidi na wasio na shukrani
Ibada ya Malipizi: Siri ya huruma kwa wenye dhambi
Kutoka Siri ya Kwanza hadi ya Pili
NYONGEZA I: Sista Lusia
anaeleza Ibada ya Malipizi ya dhambi ya Juvmamosi za Kwanza
"Hwa kamwe sijiskikii furaha kiasi ambacho ninajisikia,
kila ifikapo Jumamosi ya Kwanza"
"Hii ndivyo namna yangu ya kufanya tafakari"
NYONGEZA II: Historia
Fupi:Fatima ni Nini?
"Ahadi Kuu kwa Jumamosi Tano za Kwanza" ni sehemu
kutoka makala ya The Whole Truth About Fatima kilichoandikwa na Frère Michel de la Sainte TrinitÃ
II. Pontevedra: Matukio na
Ujumbe1
10 Desemba 1925:
Tukio la Mtoto Yesu na Mama
Yetu
Jioni ya Alhamisi, tarehe 10 Desemba, baada ya chakula cha
jioni, mpostulanti Lusia aliyekuwa na miaka kumi na minane alirejea chumbani
mwake. Hapo alitokewa na Mama Yetu na Mtoto Yesu. Hebu tusikilize maelezo
yake:2 yameandikwa katika nafsi ya tatu)
"Tarehe 10 Desemba 1925, Bikira Mtakatifu alimtokea, na
pembeni Yake, akiwa juu ya wingu linalong'aa, alikuwepo Mtoto Yesu. Bikira
Mtakatifu aliweka mkono Wake juu ya bega lake, na Alipofanya hivyo,
Alimwonyesha Moyo uliozungukwa na miiba, ambao Alikuwa ameushika katika mkono
Wake mwingine. Wakati huo huo, Mtoto Yesu alisema:
"Uwe na huruma kwa Moyo
wa Mama Yako Mtakatifu, uliozungukwa na miiba, ambayo watu wasio na shukrani
wanautoboa nayo kila wakati, na hakuna yeyote anayefanya kitendo cha malipizi
ya dhambi kuiondoa."
Baadaye, Bikira Mtakatifu alisema:
"Utazame, Binti Yangu,
Moyo Wangu uliozungukwa na miiba, ambayo watu wasio na shukrani wananitoboa
nayo Mimi kila wakati kwa kufuru zao na ukosefu wa shukrani. Wewe kwa vyovyote
jitahidi kunituliza na uwatangazie kwa jina Langu kwamba naahidi kuwasaidia
wakati wa kufa, kwa kuwapatia neema zote zinazotakiwa kwa wokovu, wale wote
ambao, kila Jumamosi ya Kwanza ya mwezi kwa miezi mitano mfululizo, wataungama,
na kupokea Komunio Takatifu, watasali matendo matano ya rozari na kuwa pamoja
nami kwa dakika kumi na tano wakitafakari mafumbo kumi na tano ya rozari kwa
nia ya kufanya Malipizi ya dhambi Kwangu."3
Tukio lilioje lenye hisia kali, na bado la unyenyekevu, lenye
maelezo yaliyo makini kama Injili yenyewe! Ni mazungumzo yaliyoje yenye
kupendeza, ambapo Mtoto Yesu na Mama Yake wanazungumza mmoja baada ya mwingine.
Mtoto Yesu kumtetea Mama, wakati Mama naye anatoa maombi yake ... ili
kuturudisha kwa Yesu.
Kama kawaida, aliyetokewa hapa anajiondoa kabisa, bila
kutuambia neno lolote kuhusu hisia zake. Je, hii sio alama ya uhakika kabisa ya
usahihi inayoyapa maelezo yake uhalisi wake? Yupo pale kuona, kusikiliza na kuelezea
kilichotokea na sio zaidi.
Na bado, ni mapenzi yaliyoje kati ya Bikira Mwenye Heri na
Mjumbe Wake! Kama vile Mtakatifu Katarina Laboure, alipokea siku ile upendeleo
wa kushikwa na Mama Yetu katika namna ya uchaji na upendo, kama ambapo mama
anapotaka kumpa mwanawe habari ya siri. Bikira Mwenye Heri aliweka mkono wake
kwenye bega la Lusia apate kutafakari Moyo uliojaa Huzuni wa Mama Yetu na
awafahamishe watu wengine.
Mwishoni, ujumbe unalingana na maneno ya ahadi kuu! Ni sawa
kama katika matukio ya 1917: ni kifupisho kilichoje cha maneno ya ahadi kuu! Ni
kifupisho kile kile kama katika Siri ya tarehe 13 Julai, ambapo hakuna neno
hata moja ambalo lingeweza kuachwa bila kuharibu mpangilio wa mawazo. Hii pia
ni alama kubwa na halisi.
Kusambazwa kwa ujumbe
Je, Lusia alifanyaje kutangaza matakwa yaliyotoka Mbinguni
yajulikane? Tunajua kuwa mara moja alimweleza yote Mama Mkuu wake, Mama
Magalhaes, ambaye aliyapokea kabisa matakwa ya Fatima na sasa alikuwa na
heshima ya dhati kwa aliyetokewa. Yeye mwenyewe alikuwa tayari kutii matakwa
kutoka mbinguni. Lusia pia alimjulisha kasisi anayewaungamisha watu katika
nyumba yao, Don Lino Garcia:"Huyu, (anavyokumbuka) aliniamuru niandike
kila kitu kuhusu (ufunuo huu) na kuyatunza maandishi haya ambayo huenda
yakahitajika."4 Lakini aliendelea kusubiri.
Lusia aliandika taarifa kamili ya yote yaliyotokea kwa kasisi
wake anayemuungamisha Monsinyori Pereira Lopes kutoka A silo de Vilar. Kwa
bahati mbaya barua hii ilipotea na tunajua kuwa ilikuwepo kwa sababu imetajwa
katika barua nyingine iliyoandikwa baadaye. Tarehe 29 Desemba Mama Magalhaes
alimfahamisha Askofu da Silva kuhusu yaliyotokea, lakini hakutoa maelezo sahihi
kabisa.5
Ndipo Lusia hatimaye alipokea jibu kutoka kwa Monsinyori
Pereira Lopes. Alionyesha kushuku, aliuliza maswali na kumshauri awe na subira.
Siku chache baadaye, tarehe 15 Februari, Lusia alimjibu akimwelezea taarifa
kamili ya yaliyotokea. Kwa bahati nzuri, barua hii muhimu kabisa imehifadhiwa
kwa ajili yetu.6 Tutayafuata maandishi haya muhimu hatua kwa hatua, tukiongezea
maneno na maoni yetu.
Kusubiri kwa mateso
"Baba Mheshimiwa Sana,
"Ningependa kwa heshima kukushukuru sana kwa barua yako
nzuri uliyoniandikia.
"Nilipoipokea na kutambua kuwa bado nisingeweza kutimiza
matakwa ya Bikira Mwenye Heri, nilijisikia uchungu kidogo. Lakini nilitambua
mara moja kuwa Bikira Mwenye Heri alinitaka nikutii.
"Hapo nilipata nafuu, na siku iliyofuata, nilipompokea
Yesu katika Komunio, nilimsomea barua yako na nilimwambia: 'Ee Yesu wangu! Kwa
neema Yako, kwa sala, kwa uchungu na matumaini, nitafanya kila jambo kwa utii
na Wewe uniangazie; mengineyo lazima Ufanye Mwenyewe.'
"Nilibakia hivyo hadi tarehe 15 Februari. Siku hizo
zilikuwa ni za uchungu mkali kwangu. Nilishangaa kama hii ilikuwa labda ni
ndoto, lakini nilijua kuwa haikuwa ndoto: Nilikuwa na hakika kuwa ilikuwa ni
jambo la kweli! Lakini bado nilijiuliza mwenyewe Bwana Wetu angekuwaje radhi
kunitokea tena, mimi niliyepokea vibaya neema nilizopewa!
"Siku niliyotakiwa kwenda kuungama ilikuwa inakaribia,
na sikuwa nimeruhusiwa kusema chochote!7 Nilitaka kumwambia Mama Mkuu lakini
shughuli zangu hazikunipa nafasi na jioni niliumwa sana kichwa. Baadaye nikiwa
naogopa kufanya makosa ya ukarimu niliwaza: 'Jambo hili litabidi kusubiri hadi
kesho yake; Nakutolea sadaka hii, Mama yangu mpenzi.' Siku hadi siku zilikwenda
hivi hadi leo.
"Tarehe hiyo ya 15, nilikuwa na kazi nyingi, na sikuwa
na mawazo hayo (ya yaliyotokea 10 Desemba) hata kidogo. Nilikuwa nakwenda nje
kutupa takataka."
Simulizi ya mwanzounaopendeza
(Novemba au Desemba 1925)
"Mahali hapo hapo, miezi michache iliyopita, nilikutana
na mtoto mdogo, ambaye nilimuuliza kama alikuwa anafahamu Salamu Maria.
Alinijibu 'Ndio', na nilimwambia aiseme ili nimsikie anavyoisema. Baada ya
kuisema mara tatu, nilimwambia aiseme peke yake, nilimwuliza kama alilijua
kanisa la Maria Mtakatifu. Alisema ndio. Halafu nilimwambia aende huko kila
siku na kusema sala hii: 'Ee Mama wa Mbinguni, nipe Mwanao Yesu!' Nilimfundisha
sala hii na baadaye niliondoka."
Hapa, kutokana na hali ilivyokuwa, Lusia ilimbidi kuelezea
kidogo kuhusu yeye mwenyewe, na matumaini yake adimu yanatufunulia kitu kuhusu
moyo wake wa ajabu.8 Karibu na mlango wa bustani anakutana na mtoto mdogo. Mara
moja anaamua kuongea naye kuhusu Bikira Maria; kumfundisha kusali. Halafu, anamtaka
kusali Salamu Maria ... kwa furaha ya kusikiliza tu.
Kwa kuwa hakuweza kusali peke yake, anasali naye mara tatu,
kulingana na mazoea ya zamani ya kusali Salamu Maria tatu kwa heshima ya Mama
Yetu. Kwa kuwa mtoto yule mdogo hakuwa tayari kusali Salamu Maria peke yake,
katekista wetu ambaye hakutaka kupoteza nafasi hii ya kumfanya Mama Yetu
afahamike na apendwe, alipendekeza njia nyingine: Alimualika kufika kwenye
kanisa la Maria Mtakatifu kila siku. Kwa kweli, Kanisa Kuu la Maria Mtakatifu
liko karibu kabisa na nyumba ya Masista wa Mtakatifu Dorothea. Je, ilikuwa muda
mfupi tu kabla au baada ya kutokewa na Mtoto Yesu tarehe 10 Desemba? Hatujui.
Hata hivyo, mpostulanti huyu mdogo alimfundisha mtoto mdogo huyu sala hii nzuri
na fupi ambayo ilikuwa ya kwake vile vile, sala yake ya kila mara na yenye
nguvu kuliko zote katika mwaka 1925. "Ee Mama yangu wa Mbinguni, nipe
Mwanao Mtoto Yesu. Na baada ya hapo aliondoka.
15 Februari 1926: Tukio jipya
la Mtoto Yesu
Maelezo ya kusisimua ya Lusia, tunayoyanukuu kwa kirefu
yanaendelea:
"Hivyo basi, tarehe 15 Februari, wakati ninarudi kama
kawaida (kutupa takataka nje ya bustani), nilimkuta mtoto mdogo pale ambaye
alionekana kufanana sawa kama yule niliyemuona kwanza, na nilimuuliza: 'Je,
ulimuomba Mama Yetu wa Mbinguni akupe Mtoto Yesu?' Yule mtoto alinigeukia na
kunijibu: 'Na wewe je, umeutangazia ulimwengu anachotaka Mama Yetu wa Mbinguni?' Na baada ya
kusema hayo akabadilika kuwa mtoto anayeng'aa.
"Hapo, kwa kutambua kuwa alikuwa ni Yesu, nilimwambia:
"Yesu Wangu! Unafahamu alivyoniambia muungamishi wangu katika barua
niliyokusomea. Alisema kuwa tukio hili ni budi litokee tena; kulitakiwa kuwa na
mambo ya uhakika ya kutufanya tuamini, na kwamba Mama Mkuu, hakuweza peke yake
kusambaza ibada hii."
"Kama ninyowaambieni
yatatekelezwa, robo nyingi zitakolewa na kutakuwa na amani ... Nitafika kuomba
... Komunio ya Malipizi ya dhambi kila Jumamosi za kwanza za mwezi."
"Ni kweli kuwa Mama Mkuu
peke yake hawezi kufanya chochote, lakini kwa Neema Yangu, anaweza kufanya kila
kitu. Itatosha kama muungamishi wako atakupa ruhusa, na pia mkuu wako atangaze
hayo ili watu wayaamini, hata kama wasipofahamu yalifunuliwa kwa nani."
"Lakini muungamishi wangu alisema katika barua yake
kwamba ibada hii tayari ipo hapa duniani, kwa sababu roho nyingi zinakupokea
kila Jumamosi ya kwanza ya mwezi kwa heshima ya Mama Yetu na wanasali mafumbo
kumi na tano ya Rozari."
"Ni kweli Binti Yangu
kuwa roho nyingi zinaanza lakini chache zinavumilia hadi mwisho, na zile
zinazovumilia zinafanya hivyo ili kupata neema zilizoahidiwa. Roho zinazotimiza
Jumamosi Tano za Kwanza kwa bidii na kufanya Malipizi ya dhambi kwa Moyo wa
Mama Yetu wa Mbinguni, zinanifurahisha zaidi kuliko zile zinazotimiza kumi na
tano lakini zikiwa baridi na hazinijali."
"Yesu Wangu, roho nyingi zinaona vigumu kuungama
Jumamosi. Je, utakubali kuungama katika muda wa siku nane?"
"Ndio, inawezekana hata
kuungama baadaye, mradi roho ziwe katika hali ya neema zinaponipokea Mimi Jumamosi
ya kwanza na ziwe zilikuwa na nia ya kufanya Malipizi ya dhambi kwa Moyo Safi
wa Maria."
"Yesu Wangu! Na roho zinazosahau kufanya nia hii je?"
"Zinaweza kufanya hivyo
katika kitubio kinachofuata zikizingatia nafasi ya kwanza ya kufanya kitubio."
"Mara baada ya hapo Alifutika pasipo mimi kupata
kufahamu chochote zaidi kuhusu matakwa ya Mbinguni hadi hivi leo."9
Hapa tena upinzani uliopo wa maandishi haya, unaondoa wale
wote wanaopinga tukio hili kwa kudai kuwa ni matokeo ya mauzauza na uwongo wa
akili iliyochanganyikiwa. Ukweli ulioelezwa — kwa namna ya kupendeza! — uko
wazi, rahisi na wa ajabu kuufanya uwe ni uwongo wa roho inayoumwa. Wakati huo
huo, unashangaza, na kuwa fumbo kwa kuuangalia mara ya kwanza tu, kuwa ni kazi
ya mwanateolojia yeyote. Ni nani angeweza kutunga maelezo ya uwongo ya aina hii
hivi hivi tu?
Kwanza kabisa, aliyetokewa amekuwa anatupa takataka za nyumba
ya watawa kila siku, kwa miezi mingi. Na anafurahi. Haelekei kuchanganyikiwa
kutokana na mazingira ya unyenyekevu ya tukio hilo. Ili kumkumbusha nia yake
kubwa kwa dunia na wokovu wa roho za watu, Mbingu ilichagua kwa usahihi muda
ule ambapo mjumbe wake alikuwa akifanya shughuli ndogo ya unyenyekevu kabisa na
iliyo duni. Zingatia vema: mtu mwenye majivuno, muongo mzoefu aliyedanganywa na
mauzauza ya kutokewa angewazia mazingira ya ajabu mno au yasiyokuwa ya kawaida,
lakini kamwe sio haya. Angeogopa kuonekana mjinga na kutoaminika. Lakini kwa
upande wake, Lusia anaelezea ukweli huu kwa namna iliyo rahisi kama vile
ulivyotokea, bila kustaajabu kuwa Mtoto Mtakatifu, aliyezaliwa katika hori la
ng'ombe alichagua mazingira haya ya unyenyekevu kujidhihirisha Mwenyewe.
Inabakia kwetu kufafanua maana halisi ya ujumbe huu wa
Pontevedra, ambao ingawaje unabakia kuwa ukamilishaji tu — au zaidi utimizaji
wa Ujumbe wa Fatima — unapelekea kuwa na umuhimu usio na kifani.
"Ni kweli Binti Yangu kuwa roho nyingi zinaanza lakini
chache zinavumilia hadi mpaka mwisho, na zile zinazovumilia zinafanya hivyo ili
kupata neema zilizoahidiwa. Robo zinazotimiza Jumamosi Tano za Kwanza kwa bidii
na kufanya Malipizi ya dhambi kwa Moyo wa Mama Yetu wa Mbinguni, zinaifurahisha
zaidi kuliko zile zinazotimiza kumi na tano lakini zikiwa aridi na hazinijali."
... Yesu akimwambia sista Lusia wa Fatima
III. Ahadi Kuu na Masharti Yake
Jambo la kushangaza kabisa kuhusu Pontevedra, ni wazi, ni ile
ahadi isiyoweza kufananishwa iliyofanywa na Mama Yetu: "kwa wale wote
ambao, kila Jumamosi ya kwanza ya miezi mitano mfululizo ..." watatimiza
masharti yote yanayotakiwa, "Naahidi kuwasaidia hao saa ya kufa kwa neema zote zinazotakiwa kwa
wokovu wa roho zao." Kwa ukarimu usio na mipaka, Bikira Mwenye Heri
anaahidi hapa neema ya neema, neema kuu kuliko zote, ile ya uvumilivu wa
mwisho. Neema hii haiwezi kupatikana hata kwa maisha yote ya utakatifu katika
sala na sadaka, kwa kuwa daima ni zawadi tu ya Huruma Takatifu. Na ahadi haina
kubagua, haina mipaka au kizuizi: "Kwa wale wote ambao ..., Naahidi."
Kutolingana kwa "ibada ndogo" inayoombwa, na neema
kubwa sana inayoambatana nayo, inatufunulia kwanza kabisa na hasa nguvu isiyo
na kikomo ya maombezi aliyopewa Bikira Maria Mwenye Heri kwa wokovu wa roho
zote. "Ahadi kuu, (Padri Alonso anaandika) kwa namna moja ni udhihirishaji
wa mapendo ya ridhaa ambayo Utatu Mtakatifu unayo kwake Bikira Mbarikiwa. Kwa
wale wanaoelewa jambo hili, ni rahisi kukubali kwamba ahadi hizi za ajabu
zinaweza kuambatana na mazoea ya unyenyekevu. Roho za aina hii zinaipokea ahadi
kwa mapendo ya mtoto kwa mama yake, na moyo mnyofu uliojaa matumaini katika
Bikira Maria Mwenye Heri."10
Kwa kifupi, tunaweza kusema kwa ukweli wote kuwa tunda la
kwanza la Komunio ya Malipizi ya dhambi ni wokovu wa yule anayeyatimiza
yaliyoagizwa. Tusiweke mipaka yoyote kwa Huruma Takatifu, bali tuzingatie ahadi
ya Bikira Maria Mwenye Heri: yeyote atakayetimiza masharti yote yaliyoagizwa
anaweza kuwa na uhakika wa kupokea wakati wa kufa angalau — na hii ni hata
baada ya nyakati za mashaka hapo nyuma katika hali ya dhambi ya mauti — neema
zinazotakiwa kupata msamaha wa Mungu na kuokolewa kutoka kwenye adhabu ya
milele.
Kama tutakavyoona, lakini, kuna kitu zaidi katika ahadi hii,
kwa sababu moyo wa kimisionari upo kila mahali katika maisha ya kiroho ya
Fatima. Ibada ya Malipizi ya dhambi pia inashauriwa kwetu kama njia ya
kuwaongoa wakosefu katika hatari kubwa kuliko zote ya kuteketea, na pia kama
njia inayofaa kuliko zote ya maombezi kwa ajili ya kupata amani duniani kutoka
kwa Moyo Safi wa Maria.11
Kama Mama Yetu alipenda kuambatanisha matunda mengi hivi
katika kuitekeleza "ibada ndogo", je, sio kwamba ili kutuvutia
tumjali kwa uhakika zaidi na kuiinua mioyo yetu ili tuifanye ibada hiyo, na
kuwafanya wengine walio nasi kuifanya kila tunapoweza? Kwa sababu hii ni muhimu
kuyajua vema masharti yaliyowekwa na kuyafahamu sawasawa.
Tangu 1925, Sista Lusia kamwe hajaacha kuyarudia na kila
wakati kwa namna ile ile. Kuna masharti matano, ambapo limeongezwa sharti la
sita linalohusu nia ya ujumla ambamo masharti mengine yaliyoombwa yanayotakiwa
yatekelezwe.
1. Jumamosi ya Kwanza ya miezi
mitano mfululizo
"Wale wote ambao, Jumamosi ya kwanza ya miezi mitano
mfululizo ..." Sharti la kwanza la Mbinguni halina sheria wala kanuni au
hata chochote ambacho ni kipya kabisa. Linakwenda vema na desturi ya tangu
zamani ya Kikatoliki ya kumcha Mungu, ambapo wakati siku za Ijumaa hufanywa
ibada ya kumbukumbu ya Mateso ya Yesu Kristu na kuuheshimu Moyo Wake Mtakatifu,
inafaa kabisa kufanya ibada Jumamosi kwa Mama Yake Mtakatifu. Ndivyo ilivyo
desturi iliyo na heshima ambayo ilisababisha kuchaguliwa kwa siku ya Jumamosi.
Lakini hii haitoshi: kama tukiangalia kwa makini, sharti
kubwa la Pontevedra linaonekana kama ukamilifu wa furaha wa mzunguko mzima wa
ibada. Ulianza wenyewe, halafu ulitiwa nguvu na kupangwa kisheria na Roma, na
inaelekea yote haya ni matayarisho yaliyoongozwa na Mungu kwa yale ambayo
yangetokea baadaye.
Jumamosi Kumi
na Tano kwa heshima ya Mama Yetu wa Rozari Takatifu. "Kwa muda mrefu, washiriki wa vyama mbalimbali vya
Rozari walikuwa na desturi ya ibada ya Jumamosi kumi na tano mfululizo kwa
Malkia wa Rozari Takatifu, kabla ya sikukuu hii, au wakati mwingine katika
mwaka. Katika kila Jumamosi ya namna hii, walizisogelea karibu sakramenti na
kufanya ibada za kumcha Mungu kwa heshima ya mafumbo kumi na tano ya
Rozari." Mwaka 1889, Baba Mtakatifu Leo wa 13 aliwajalia waamini wote
rehema kamili kwa kila moja ya Jumamosi hizi kumi na tano mfululizo. Mwaka
1892, "pia aliwaruhusu wale walioshindwa kihalali siku ya Jumamosi, uwezo
wa kufanya ibada hiyo siku za Jumapili, bila kupoteza rehema." 12
Jumamosi Kumi na Mbili za
Kwanza za mwezi. Kwa idhini ya Baba Mtakatifu Pius wa 10, ibada ya Jumamosi za kwanza za mwezi imekubaliwa
rasmi: "Waumini wote, ambao kila Jumamosi ya kwanza au Jumapili ya kwanza
ya miezi kumi na mbili mfululizo, wanafanya ibada kwa sauti au kimoyomoyo kwa
muda fulani kwa heshima ya Bikira Safi kwa kutunga kwake mimba, wanapata rehema
kamili kwa kila moja ya siku hizo. Masharti: Kufanya kitubio, kupokea Ekaristi
na sala kwa ajili ya nia za Baba Mtakatifu." 13
Ibada ya Malipizi ya dhambi
kila Jumamosi ya Kwanza ya mwezi. Mwishowe, tarehe 13 Juni 1912, Baba Mtakatifu Pius wa
10 alitoa rehema mpya kwa ibada ambazo zilitangulia karibu sawasawa na maagizo
ya Pontevedra: "Kuamsha uchaji wa Waamini kwa Moyo Safi wa Maria, Mama wa
Mungu, na kufanya Malipizi ya dhambi kutokana na uovu unaofanywa na watu wabaya
kwa Jina lake Takatifu na Majaliwa Yake, Baba Mtakatifu Pius wa 10 alitoa kwa
Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi, rehema kamili inayotumika kwa roho zilizo
Toharani. Masharti: kufanya kitubio, kupokea Ekaristi, sala kwa ajili ya nia za
Baba Mtakatifu, na ibada za uchaji kwa lengo la Malipizi ya dhambi kwa heshima
ya Bikira Safi Kabisa."14 Miaka mitano baada ya siku hii ya tarehe 13 Juni
1912, palitokea huko Fatima ufunuo wa Moyo Safi wa Maria, "ukiwa
umezungukwa na miiba iliyoonekana kuutoboa." Sista Lusia alisema baadaye:
"Tulifahamu kwamba ulikuwa ni Moyo Safi wa Maria uliojeruhiwa na dhambi za
watu uliamuru Malipizi ya dhambi."15
Tarehe 13 Novemba 1920, Baba Mtakatifu Benedikto wa 15 alitoa
rehema mpya kwa ibada ya namna hii ilipotimizwa katika Jumamosi za miezi minane
mfululizo. 16
Desturi ya Ibada ... Inapendeza
jinsi gani kuona Mbingu inaridhika kwa kuuwekea taji ushirika wa uchaji wa
Kikatoliki, ikidhihirisha usahihi wa maamuzi ya Baba Mtakatifu, na Baba
Mtakatifu wa aina yake, Baba Mtakatifu Pius wa 10! Kwa njia hiyo hiyo, Bikira
Mwenye Heri alikuja Lurdi kuthibitisha maagizo yasiyo na makosa ya Baba
Mtakatifu Pius wa 9.
Hebu pia tuseme jambo hili sasa hivi: katika kumtaka Baba
Mtakatifu akubali kwa heshima ibada ya Malipizi ya dhambi iliyofunuliwa
Pontevedra, Mama Yetu hakuwa anaomba jambo lolote ambalo haliwezekani. Maongozi
ya Mungu yalikuwa yamekwishatayarisha kila kitu vizuri kwa jinsi ambayo mnamo
1925 - 1926, ibada hii ilikuwa sambamba kabisa na mfululizo wa maamuzi ya Baba
Mtakatifu yahusuyo utekelezaji wa ibada ya Jumamosi ya kwanza.
Bado ni Ibada mpya sana ... Lakini, mambo
gani mapya yaliyomo, katika ujumbe huu wa Pontevedra! Na kwanza kabisa, katika
utoaji wa uwezo kupita kiasi ambao Mbingu tu ndio ina uhuru wa kuutoa: tarehe
10 Desemba, Bikira Maria hahitaji tena kufanyiwa ibada ya Jumamosi kumi na
tano, kumi na mbili au nane. Anajua kigeugeu chetu, na anaomba Jumamosi tano
tu, zinazolingana na mafungu ya Rozari.
Halafu, zaidi ya yote, ahadi inayoambatana nayo imeongezeka
kwa kiasi kikubwa: sio tena suala la rehema (yaani, maondoleo ya adhabu kwa
dhambi ambazo tayari zimekwishasamehewa), lakini neema inayoonyesha zaidi,
uhakika wa kuzipata saa ya kufa "neema zote zinazohitajika kwa
wokovu." Ahadi nzuri zaidi kuliko hii isingeweza kupatikana, ukizingatia
kuwa inahusu kufaulu au kushindwa katika "suala muhimu kuliko yote, suala
letu pekee: suala kubwa la wokovu wetu wa milele."17
2. Kitubio
Tumeona ya kwamba si lazima kitubio kifanywe ile Jumamosi ya
kwanza. Kama ni kutokana na sababu za msingi, kinaweza kufanywa baada ya siku
nane, lakini ili mradi kuwe na kitubio japo kila mwezi. Lakini, ni dhahiri
kuwa, kwa kadiri inavyowezekana, ni vema zaidi kitubio kifanywe siku
inayokaribiana na Jumamosi ya kwanza.
Wazo la kufanya Malipizi kwa Moyo Safi wa Maria lazima vile
vile liwepo. Kwa njia hii, anasema Padri Alonso, "roho inaongezea kwenye
sababu kuu ya majuto kwa dhambi zetu - ambapo daima itakuwa kwamba dhambi ni
kumkosea Mungu, ambaye ametukomboa kwa njia ya Kristu — sababu nyingine ya
majuto ambayo bila shaka itatufanya tuwe na mwongozo unaofaa: majuto kwa makosa
tuliyoyafanya kwa Moyo wa Huzuni na Safi wa Bikira Maria."18
3. Komunio ya Malipizi ya
dhambi katika Jumamosi za Kwanza.
Komunio ya Malipizi ya dhambi, ni wazi, ni sehemu muhimu
kuliko zote ya ibada ya Malipizi ya dhambi. Matendo mengine yote yanaitegemea
ibada hii. Ili kuelewa maana na kusudi lake, lazima itazamwe kwa uhusiano na
Komunio ya muujiza ya mwishoni mwa mwaka 1916; tayari Komunio hii ilikuwa
imeelekezwa moja kwa moja kwenye wazo la Malipizi ya dhambi,19 tunashukuru kwa
maneno ya Malaika. Ibada ya Malipizi ya dhambi lazima pia itazamwe kwa uhusiano
na Komunio ya Ijumaa tisa za Kwanza za kila mwezi zilizoagizwa na Moyo
Mtakatifu wa Yesu huko Paray-le-Monial.
Mtu angeweza kupinga kwamba kupokea Ekaristi katika kila
Jumamosi ya kwanza ya miezi mitano mfululizo ni jambo gumu sana kwa wengi wa
Waumini, ambao hawana Misa katika parokia yao siku hiyo ... Ni swali la namna
hiyo hiyo Padri Gonçalves, kasisi muungamishi wa Lusia, alimuuliza katika
barua aliyomwandikia tarehe 29 Mei 1930:
"Ikiwa mtu hawezi masharti yote siku ya Jumamosi, je
inawezekana kufanya hivyo siku ya Jumapili? Watu wa vijijini kwa mfano,
hawawezi kufanya hivyo mara nyingi kwa kuwa wanaishi mbali sana ..."20
Bwana Wetu alitoa jibu kwa Sista Lusia usiku wa tarehe 29-30
Mei 1930: "Kufanya ibada ya namna hii kutakubaliwa vile vile siku ya Jumapili
inayofuatia Jumamosi ya kwanza wakati mapadri Wangu, kwa sababu halali,
wanawaruhusu watu."21
Kwa hiyo, sio Komunio tu, bali hata pia kusali Rozari na
kutafakari mafumbo matano, kunaweza kufanyika siku ya Jumapili, kwa sababu
halali ambazo mapadri wameachiwa kuamua. Ni rahisi kuomba ruhusa ya namna hii
wakati wa kuungama. Angalia tena tabia ya kanisa Katoliki ya Ujumbe wa Fatima.
Ni kwa mapadri Wake, na sio kwa dhamira ya mtu, ndipo Yesu anawapa madaraka ya
kutoa ruhusa hii ya nyongeza.
Baada ya ruhusa nyingi namna hii, nani bado angeweza kudai
kuwa alishindwa kutimiza maagizo ya Bikira Maria?
4. Kusali Rozari
Katika kila moja ya matukio sita ya 1917, Mama Yetu
aliwaagiza watu kusali Rozari kila siku. Kwa kuwa ni suala la kutubu makosa
yaliyofanyiwa Moyo Safi wa Maria, ni sala gani nyingine inayosemwa ingeweza
kumpendeza kuliko hii?21
5. Tafakari ya dakika kumi na
tano ya Mafumbo Kumi na Tano ya Rozari.
Kwa nyongeza katika kusali Rozari, Mama Yetu anaagiza dakika
kumi na tano za tafakari juu ya mafumbo kumi na tano ya Rozari. Hii haina
maana, ni wazi, ya kwamba robo saa inatakiwa kwa kila fumbo! Robo saa tu
inatakiwa kwa mafungu yote! Wala sio lazima kutafakari kila mwezi juu ya
mafumbo haya kumi na tano. Lusia anamwandikia Padri Gonçalves: "Kuwa
pamoja na Mama Yetu kwa dakika kumi na tano huku ukitafakari juu ya mafumbo ya
Rozari." Kwa mama yake, Maria Rosa, Lusia alimwandikia kitu chenye asili
hiyo hiyotarehe 24 Julai 1927, akimshauri kutafakari baadhi ya mafumbo, ambayo
yuko huru kuyachagua:
"Mama, ningependa pia unipe kitulizo cha kuzingatia
ibada ambayo najua inampendeza Mungu na ambayo Mama yetu mpenzi wa Mbinguni
ndiye aliyeiomba. Kwa hiyo, mara tu nilipoifahamu, nilitamani kuizingatia na
kuona kuwa dunia nzima inaizingatia.
"Kwa hiyo, mama, natumaini kuwa utanijibu kwa kusema
kwamba utaifanya, na pia jitahidi kuwafanya wengine wote huko kuizingatia.
Usingeweza kunipatia kitulizo kikubwa zaidi kuliko hicho.
"Kinachotakiwa tu ni kufanya kama ilivyoandikwa katika
picha hii ndogo. Kitubio kinaweza kufanywa siku nyingine, isiyokuwa Jumamosi.
Dakika kumi na tano (za tafakari) ninavyodhani zinaweza kukusumbua, lakini ni
rahisi mno. Nani angeona ugumu kuwaza juu ya mafumbo ya Rozari? Kutafakari juu
ya Malaika kumpasha habari Maria na unyenyekevu wa Mama yetu mpenzi, ambaye
alipojiona ametukuzwa kiasi hicho, anajiita mwenyewe Mtumishi wa Bwana; katika
Mateso ya Yesu, Ambaye aliteseka mno kwa ajili ya mapendo kwetu; na juu ya Mama
Yetu Mtakatifu alipokuwa karibu na Yesu pale Kalvari? Nani asingeweza kutumia
dakika kumi na tano katika mawazo haya matakatifu, pamoja na Mama mwenye huruma
kuliko wengine wote?
Kwaheri, mama mpenzi. Mtulize kwa njia hii Mama wa Mbinguni,
na jitahidi kuwafanya wengine wengi kumtuliza kwa njia hiyo hiyo. Kwa namna hii
utanipa pia mimi mwenyewe furaha isiyo na kifani...
"Binti yako akupendaye sana, anayebusu mkono
wako."23
Katika barua hii nzuri, Sista Lusia anasisitiza sharti la
sita, ambalo ndilo kuu: kila moja ya ibada hizi lazima itimizwe "kwa moyo
wa Malipizi ya dhambi" kwa Moyo Safi wa Maria: "mtulize kwa njia hii
Mama wa Mbinguni..." aliandika.
6. Nia ya kufanya Malipizi ya
dhambi: "Wewe, angalau jitahidi kunituliza Mimi."
Bila nia hii kuu, bila nia hii ya mapendo inayotamani kufanya
Malipizi ya dhambi kwa Mama Yetu ili kumtuliza, ibada hizi nyingine zote nje ya
hii, zenyewe peke yake hazitoshi kuipata ahadi kuu. Hii ni wazi.
Ibada ya Komunio ya Malipizi ya dhambi lazima ifanywe kwa
makini na kwa bidii. Bwana Wetu alielezea jambo hili kwa Sista Lusia
alimpomtokea tarehe 15 Februari 1926: "Ni kweli, Binti Yangu, kuwa roho
nyingi zinaanza (ibada ya Jumamosi kumi na tano), lakini chache tu zinavumilia
hadi mwisho, na zile zinazovumilia zinafanya hivyo ili kupokea neema
zilizoahidiwa. Roho zinazotimiza Jumamosi Tano za Kwanza kwa bidii na kufanya Malipizi
ya dhambi kwa Moyo wa Mama yako wa Mbinguni zinanifurahisha zaidi kuliko zile zilizo baridi na
kutojali zinazotimiza kumi na tano..."24 Mama Yetu anaomba kidogo tu
lakini kwa ukamilifu ili tujitolee wenyewe kutoka moyoni. Hii haina maana kuwa
daima itakuwa ni kwa bidii ile ile kulingana na kanuni kuu ya imani ya kiroho:
"Kuamua kupendani kupenda."
Mama Yetu wa Fatima tarehe 13 Oktoba 1917 alishika Skapulari
Yake ya Mlima Karmeli akitukumbusha kwa heshima juu ya ahadi Yake: "Chukua
Skapulari hii, Yeyote atakayekufa akiwa ameivaa hatateseka katika moto wa
milele. Itakuwa ni ishara ya wokovu, kinga katika hatari, na ahadi ya amani."
Angalia Garment of Grace ukurasa wa 43
Maneno mafupi ya Mtoto Yesu na Mama Yetu tarehe 10 Desemba
1925, yanatueleza yote. Yanatosha kutufanya tuelewe nia ya kweli ya ibada hii
ya Malipizi ya dhambi:
"Utazame, Binti Yangu,
Moyo Wangu umezungukwa na miiba, ambayo watu wasio na shukrani wananitoboa nayo
kila wakati kwa kufuru zao na kukosa shukrani...bila kuwepo mtu yeyote
anayefanya ibada ya Malipizi ya dhambi ili kuiondoa...Wewe, angalau, jitahidi
kunituliza Mimi."
Mfano huu ambao una maana sana, unaelezea kila kitu: kufuru
na ukosefu wa shukrani wa wenye dhambi ni kama miiba mingi sana mikali, ambayo
sisi tu tunaweza kuiondoa kwa matendo yetu ya mapendo na Malipizi ya dhambi.
Kwani mapendo na "huruma", ndio roho ya ibada zote hizi. Ni jambo la
kuutuliza Moyo Safi wa "mama mwenye huruma kuliko wengine wote" ambao
umejeruhiwa sana.
Lusia alikuwa ameelewa jambo hili vema wakati ule ule. Mwisho
wa barua yake kwa Monsinyori Pereira Lopes, anaposimulia kutokea kwa Mtoto Yesu
tarehe 15 Februari 1926 ni ushahidi fasaha wa ukweli huu:
"Mara moja baadaye, alifutika bila mimi kufahamu lolote
zaidi juu ya matakwa ya Mbinguni adi hivi sasa.
"Na kulingana na matakwa yangu, (anaendelea) ningependa
moto wa mapendo makuu uwashwe katika roho za watu, ili kwa kudumisha mapendo
haya, waweze kweli kuutuliza Moyo Mtakatifu wa Maria. Angalau ninayo nia ya
kumtuliza kwa kiasi kikubwa Mama yangu mpenzi wa Mbinguni, kwa kuteseka sana
kwa ajili ya mapendo Yake."25
Uhalisi wa ujumbe huu lazima usisitizwe.26 Kwa kuwa hapa
hakuna suala, angalau hasa, la kumtuliza Bikira Mwenye Heri kwa kuwa na huruma
kwa Moyo Wake uliojeruhiwa na mateso ya Mwanaye. Ili kuwa na uhakika, Ujumbe wa
Fatima unachukulia mtazamo huu wa uchaji waKikatoliki ambao tayari ni desturi.
Tarehe 13 Oktoba 1917, Mama Yetu wa Mateso Saba alitokea angani kwa wachungaji
watatu.27 Lakini, maana sahihi kuliko zote ya ibada ya malipizi ya dhambi
iliyoagizwa Pontevedra haihusu zaidi tafakari juu ya mafumbo ya huzuniya Rozari
kama kutafakari juu ya maovu yanayotendwa hivi sasa kwa Moyo Safi wa Maria
kutoka kwa watu wasio na shukrani na watu wanaokufuru wanaokataa upatanishi
wake wa kimama na kudharau mamlaka yake ya ki-Mungu.* (*MUHTASARI WA MWANDISHI:
Bikira Maria Mbarikiwa, ingawaje ni kiumbe tu, kwa sababu Mungu amemfanya kweli
Mama wa sMungu na Malkia wa Mbingu, ana haki ya kusemwa kuwa ana m'amlaka ya
ki-Mungu.) Yote haya ni miiba mingi sana ambayo lazima iondolewe kutoka kwenye
Moyo Wake kwa njia ya ibada zamapendo za Malipizi ya dhambi kumtuliza, na pia
kupata msamaha kwa roho ambazo zimekuwa na ujasiri wa kumtendea maovu kwa kiasi
kikubwa sana.
Hakuna jambo ambalo lingeweza kutufanya kuelewa vizuri zaidi
moyo wa kweli wa Malipizi ya dhambi ilivyoagizwa na Mama Yetu wa Fatima kuliko
maelezo ya ufunuo muhimu aliojaliwa Sista Lusia tarehe 29 Mei 1930.
IV. Nia ya Ibada ya Malipizi
ya dhambi:
Ufunuo wa 29 Mei 1930
Sista Lusia wakati huo alikuwa Tuy. Muungamishi wake, Padri
Gonçalves, alikuwa amempa maswali kadhaa kimaandishi. Hapa, hebu tujikumbushe
lile la nne tu: "Kwa nini Jumamosi tano, (aliuliza) na sio tisa, au saba,
kwa heshima ya mateso ya Mama Yetu?"28 Jioni ile ile, Lusia alimsihi Bwana
Wetu kumuangazia na jibu kwa maswali haya. Siku chache baadaye, alimjibu
muungamishi wake29 Yafuatavyo:
"Nilipokuwa kanisani pamoja na Bwana Wetu usiku wa 29-30
Mei 1930 (tunajua kuwa ilikuwa tabia yake kufanya saa takatifu kuanzia saa tano
hadi sita usiku, hasa jioni ya siku za Alhamisi, kulingana na matakwa ya Moyo
Mtakatif huko Paray-le-Monial), na nilipoongea na Bwana Wetu kuhusu swali la
nne na la tano, kwa ghafla nilijihisi mimi mwenyewe kujawa na Utakatifu
Uliokuwepo na, kama sikosei,29a haya ndiyo yaliyofunuliwa kwangu:
"Binti Yangu, sababu ni
rahisi. Kuna aina tano za makosa na kufuru yanayofanywa dhidi ya Moyo Safi wa
Maria:
1) Kufuru dhidi ya imani kuwa
Bikira Maria alitungwa mimba pasipo dhambi ya asili.
2) Kufuru dhidi ya Ubikira
wake wa Daima.
3) Kufuru dhidi ya Umama Wake
wa Mungu, na kukataa wakati huo huo kumtambua kama Mama wa watu.
4) Kufuru za watu ambao
hadharani wanapanda katika mioyo ya watoto kutojali, dharau, au hata chuki kwa
Mama huyu Safi.
5) Makosa ya wale ambao
wanaomdhihaki moja kwa moja katika sanamu zake takatifu.
"Hii, Binti Yangu, ndiyo
sababu kwa nini Moyo Safi wa Maria ulinisukuma Mimi kuomba ibada hii ndogo ya
Malipizi ya dhambi..."30
Miiba ya Moyo Safi wa Maria
Hapa hebu tumfuate Padri Alonso, kwani katika uchunguzi wake
wa ujumbe wa Pontevedra, anaandika ufafanuzi mrefu na wa maana juu ya maovu
matano dhidi ya Moyo Safi wa Maria yaliyotajwa na Bwana Wetu. Kufuru za wapotoshaji dini,
watu waliofarakana na watu wanaomdharau Mungu
Tukiwa tumepofushwa na udanganyifu wa ulimwengu, tumekuwa na
mwelekeo tangu 1962 wa kusahau kwamba kuna ukweli ulio wazi unaokumbushwa hapa
katika Ujumbe wa Fatima: wale ambao kwa ukaidi na kwa kufahamu kabisa wazi wazi
wanakataa mamlaka ya Bikira Maria Mwenye Heri, wanafanya kufuru za kuchukiza
kuliko zote kwa upande Wake.
Kufuru ya kwanza:
Dhidi ya imani ya kuwa Bikira Maria alizaliwa pasipo dhambi
ya asili. Padri Alonso anauliza: ni watu gani wanaotenda maovu haya dhidi ya
Moyo Safi wa Maria? Jibu halina mashaka yoyote: "Kwanza kabisa na kwa
ujumla madhehebu ya Kiprotestanti yanayokataa kukubali kanuni ya imani
iliyotafsiriwa na Baba Mtakatifu Pius wa 9 na ambayo yameendelea kushikilia
kwamba Bikira Mwenye Heri alizaliwa na dhambi ya asili na hata dhambi za
binafsi. Vivyo hivyo inaweza kusemwa kwa Wakristu wa Mashariki, kwani licha ya ibada
zao kubwa za Maria, wao pia wanaikataa imani hii."31
Sista Lusia wa Fatima anasimulia Maono ya Jehanamu kama
ifuatavyo: "Tuliona kama vile bahari kubwa mno ya moto, ambamo ndani yake
mlikuwa mmetupwa, mashetani na roho zilizokuwa na miili ya kibinadamu kama
majivu maangavu, wakiwa weusi na walioungua. Wakinyanyuliwa juu angani kwa
mionzi ya moto, walianguka chini pande zote, kama cheche katika moto mkubwa,
bila uzito au mwendo, katikatik ya violio vikubwa na milio ya maurnivu na
kukata tamaa iliyotufanya tuogope sana na kutetemeka kwa woga. Mashetani
walitofautishwa kwa kuwa na maumbile ya kutisha na ya kucjiloza ya wanyama
wasiojulikana, kama majivu ya moto, meusi lakini maangavu Maono haya yalichukua
muda mfupi tu, na lazima tumshukuru Mama Yetu wa Mbinguni aliyekuwa ametutayarisha
kabla kwa kutuahidi kutuchuka pamoja naye Mbinguni: la sivyo naamini kwamba
tungekufa kutokana na woga na kitisho." Mama Yetu alisema: "Mmeiona
Jehanamu ambako roho za wenye dhambi masikini zinakwenda, ili kuziokoa, Mungu
anataka kuanzisha ulimwenguni ibada kwa Moyo Wangu Safi." Angalia pia
ukurasa wa 24.
Kufuru ya pili: Ingawaje
Waothodoksi wanaikubali, wengi wa Waprotestanti pia wanaukataa ubikira kamili
na wa daima wa Maria, "kabla, wakati na baada ya kuzaa."
Kufuru ya tatu: Ingawaje
kinadharia wanaukubali Umama wa Mungu wa Maria ilivyotafsiriwa na Mtaguso wa
Ephesus, wanakataa kumkubali kama Mama wa watu katika maana ya Kikatoloki,
ambayo inamhusisha na ukombozi na nafasi yake kama Mpaji wa neema.
Kufuru ya nne: inahusu
kupotosha kwa watoto kunakofanywa na maadui wa Mama Yetu ambapo wanajitahidi
kuwafundisha kutojali, dharau na hata chuki kwa Bikira Safi,na ya tano, ambapo
wanamchukiza katika sanamu zake. Dhambi hizi mbili za mwisho ni matokeo
yanayotokana na zile tatu za kwanza, na mara nyingi zinakwenda pamoja. Uvunjaji
wa sanamu, au angalau kukataa kwa ukaidi teolojia ya Kikatoliki juu ya sanamu,
bado kabisa hakujafutika.
Kwa kifupi katika muda wa karne tatu na nusu Wapinga Kanisa
wamekuwa wakifanya juhudi kubwa na isiyoisha dhidi ya Bikira Mwenye Heri, dhidi
ya kuongezeka kwa Ibada Kwake, dhidi ya kutawala Kwake katika mioyo ya watu na
katika jamii zote. Katika kufuata nyayo za Uprotestanti, kufuatia Ujanseni na
dharau baridi kwa ibada ya kweli kwa Bikira Mtakatifu, akili za binadamu za karne
ya kumi na nane na kumi na tisa, pamoja na mambo ya kisasa ya karne ya
ishirini, vinaendelea kuyashambulia mafundisho ya dini na ibada kwa Maria, na
tena kwa madharau na kwa uwongo. Mwishowe, ni jambo linalofahamika kwa wote
jinsi ukomunisti wa Bolshevik ulivyojaribu kwa kila njia iliyowezekana kuharibu
heshima kubwa kwa Mama wa Mungu, iliyokuwa imezama ndani ya mioyo ya watu wa
Urusi. Sanamu takatifu ziliondolewa kwa kuharibiwa au kuzificha ... na bado
zinasubiri siku ya furaha zaidi, itakaporuhusiwa kuziheshimu tena.
Kufuru za watoto wakaidi na
wasio na shukrani. Lakini kuna jambo ambalo ni baya zaidi, la hatari zaidi
kwa mbali kuliko maovu yote ya wapotoshaji dini, watu waliofarakana, waasi dini
na watu wanaomdharau Mungu. Ni kufuru za watoto wa Kanisa lenyewe dhidi ya Moyo
Safi wa Maria. Kadiri muda unavyokwenda, ujumbe wa Pontevedra unaonekana kuwa
ni utabiri wa kinabii.
Padri Richard, kiongozi wa Blue Army nchini Ufaransa na
ambaye usingeweza kumdhania awe na tabia ya kuona kila kitu ni kibaya, anazungumzia
juu ya jambo hili: "Nani angeweza kufikiri miaka hamsini iliyopita kwamba
maovu haya matano dhidi ya Maria yangesambaa ndani ya viongozi wa Kanisa
Katoliki lenyewe, na kwamba idadi kubwa ya watoto wanaobatizwa na kufundishwa
katika parokia zetu wangeshindwa kusema sala ya "Salamu Maria".32
Padri Alonso alilazimika kutoa maoni yanayofanana na hayo.
Hali hii imeenea leo kiasi kwamba ufafanuzi wowote unakuwa ni
kazi bure. Kuna baadhi ya wanateolojia, baadhi ya mapadri, baadhi ya maaskofu
ambao wana makosa katika kufuru hizi tano. Sio kwamba kuna mifano michache ya
pekee, lakini mamia na labda hata maelfu. Haitoshi kuuchunguza ukweli huu. Ni
lazima tugundue chanzo chake na kuelezea tumefikaje mahali hapa. Padri Alonso
angalau alilielezea jambo hili kwa usahihi: "Enzi kubwa ya Maria" iliyozinduliwa mwaka 1854 kwa tafsiri ya
kanuni ya imani ya Bikira Maria kuzaliwa pasipo dhambi ya asili, anadiriki
kuandika, ilifungwa kutokana na Mtaguso wa Pili wa Vatican.33 Lakini hii
ilitokeaje? Na kwa nini kushuka huku katika ibada ya Maria, ambayo ilikuwa
imeshamiri kwa wingi wakati wa kifo cha Baba Mtakatifu Pius wa 12? Hili ndilo
jambo itatubidi tulichunguze baadaye, katika mtazamo wa Siri ya Tatu.
Hata hivyo, hebu tuseme hivi sasa kwamba jambo la kwanza
katika Ujumbe wa Fatima ni imani — hasa, imani ya kanuni ya dini. Ibada ya
kweli kwa Bikira Mbarikiwa daima na lazima itanguliwe na imani katika majaliwa
na mamlaka Yake kama yalivyotafsiriwa bila makosa na Baba Mtakatifu au
yalivyofundishwa na akili ya kawaida na kukubaliwa kwa pamoja kwa karne nyingi
na Waumini. Ni kweli pia kwamba dhambi kubwa kuliko zote dhidi ya Bikira
Mtakatifu kwanza kabisa ni dhambi dhidi ya imani. Fundisho hili muhimu ni
lazima liwekwe akilini.
Ibada ya Malipizi ya dhambi:
siri ya huruma kwa wenye dhambi
Baada ya kuzitaja kufuru tano anazotendewa Mama Yake
Mtakatifu, Bwana Wetu alimpa Sista Lusia maelezo dhahiri yanayotuwezesha
kupenya ndani ya siri ya Moyo Wake Safi, unaotiririka huruma kwa wenye dhambi
wote, hata wale wanaomdharau na kumchukiza.
"Tazama, Binti Yangu, nia
ambayo Moyo Safi wa Maria ulinisukuma kuomba ibada hii ndogo ya Malipizi ya
dhambi, na kwa kuitilia maanani, ni kutoa huruma Yangu kuzisamehe roho
zilizokuwa na bahati mbaya ya kumkosea. Kwa upande wako, daima jitahidi bila
kuchoka kwa sala na sadaka kuifanya huruma Yangu izihurumie hizi roho
masikini."34
"Dhambi dhidi ya Roho
Mtakatifu." Hapa tuna moja ya mambo makuu ya Ujumbe wa Fatima: Kwa
kuwa Mungu ameamua kudhihirisha zaidi na zaidi mpango Wake mkuu wa mapendo, ambao
ni kuwapa watu neema kupitia upatanishi wa Bikira Mbarikiwa, inaonekana kuwa
kukataa kwao kukubali kwa utii kile anachotaka Mungu ni kosa ambalo linaujeruhi
Moyo Wake kuliko mengine yote, na ambalo haoni Yeye Mwenyewe jinsi ya
kulisamehe. Dhambi hii inaonekana haisameheki, kwa sababu kwa Mkombozi Wetu
hakuna kosa lingine lisiloweza kusameheka kuliko lile la kumdharau Mama Yake
Mtakatifu, na "kuuchukiza Moyo Wake Safi, ambao ni makao ya Roho
Mtakatifu. Hii ni kufanya 'kufuru dhidi ya Roho Mtakatifu kosa ambalo
halitasamehewa katika ulimwengu huu au ule ujao.'35
Katika mwaka 1929, katika tukio la Tuy ambalo ni timilisho la
mwisho la Fatima, Mama Yetu anamalizia kudhihirishwa kwa namna ya ajabu kwa
Utatu Mtakatifu kwa maneno haya ya kushangaza: "Ni roho nyingi sana ambazo Haki ya Mungu inaziadhibu kwa dhambi
zinazotendwa dhidi Yangu, hivyo basi, nakuja kuomba ibada ya Malipizi ya
dhambi. Jitolee sadaka wewe mwenyewe kwa nia hii na usali." Maneno haya
ni makubwa kiasi kwamba watu kadhaa wanaotafsiri walijichukulia uhuru wa
kuipunguza maana yake.36
"Tendo dogo la Malipizi
ya dhambi" kuwaokoa wakosefu wakubwa kuliko wote. Ndiyo, Mama
Yetu anathibitisha kwa uchungu, roho nyingi zinapotea kwa ajili ya dharau zao,
kufuru zao dhidi Yake ... Kwa namna hii, kutupa mfano wa kuwapenda maadui zetu,
Yeye Mwenyewe anaingilia kati, kwa sababu Yeye peke yake bado anaweza kuwaokoa
hawa wakorofi na wenye majivuno na kukosa shukrani ambao walimuasi. Kama
"Mama wa Huruma na Mama wa Msamaha", kama tunavyoimba katika Salve
Mater, anatuombea sisi mbele ya Mwanaye: ibada ya Mama kwa mtoto ya roho zenye
imani, na Komunio za Malipizi ya dhambi zinazotolewa katika Jumamosi Tano za
Kwanza za mwezi kuutuliza Moyo Wake uliochukizwa, zipokelewe naye katika
Malipizi ya dhambi kwa makosa ya wadhambi. Mama Yetu anaomba ili akubali
kuipokea hii "ibada ndogo", na kulichukulia maanani hili "tendo
dogo" la Malipizi ya dhambi kwa Moyo Wake Safi, na akubali kutoa msamaha
licha ya mengine yote, kwa wakosa shukrani na wanaokufuru, roho zote masikini ambazo
zimekuwa na ujasiri wa kumkosea Yeye — Yeye, Mama Yake Mtakatifu!
Na kama ilivyo daima, Bwana Wetu anamfanyia Yeye Mama Yetu
jinsi anavyotaka. Kwa njia hii Bwana Wetu Yesu Kristu anaifanya ibada ya
Malipizi ya dhambi njia ya uhakika na ya kufaa ya kuziongoa roho, roho nyingi
kati ya zile zilizo katika hatari kubwa kuliko zote ya kupotea milele.
Inatubidi kunukuu hapa maandishi muhimu ambamo "ahadi kuu" yenyewe ni
jambo dogo, linalojiondoa lenyewe ukilinganisha na nia kuu ya Moyo wa Maria,
ambayo ni wokovu wa wenye dhambi wote. Mwezi Mei 1930, Sista Lusia alimwandikia
Padri Gonçalves:
"Inaonekana kwangu kwamba Bwana mwema, ndani kabisa ya
moyo wangu, anasisitiza kuwa nimuombe Baba Mtakatifu atoe kibali kwa ibada ya
Malipizi ya dhambi, ambayo Mungu Mwenyewe na Bikira Mtakatifu wamejishusha
kuiagiza mwaka 1925. Kwa kutilia maanani ibada hii ndogo, Wanataka kutoa neema ya msamaha kwa
roho ambazo zimekuwa na bahati mbaya ya kuukosea Moyo Safi wa Maria, na Bikira
Mtakatifu anaahidi kwa roho ambazo zitafanya Malipizi ya dhambi Kwake,
kuwasaidia saa ya kufa kwa neema zote zinazohitajika kwa kuziokoa."37
Malipizi ya dhambi ni lazima. Kuokoa roho,
roho zote, "hasa zile zinazohitaji msaada kuliko nyingine zote",
kuziokoa kutoka kwenye moto wa milele unaotaka kuziangamiza, ndiyo katika mambo
yote, nia kuu ya ibada ya Jumamosi za kwanza za mwezi, kama vile nia hiyo hiyo
ilivyokwishaonyeshwa na Mama Yetu tarehe 19 Agosti 1917, akiwaalika kwa haraka
wachungaji watatu kusali na kutoa sadaka: "Salini, salini sana na toeni
sadaka kwa ajili ya wenye dhambi, kwa kuwa roho nyingi zinakwenda motoni kwa
sababu hazina mtu yeyote wa kusali na kutoa sadaka kwa ajili yao."
Bikira Maria Mwenye Heri amefanywa kuwa Mpatanishi wa
ulimwengu na Mama wa Neema ya Mungu. Hata hivyo, kwa mpango wa Maongozi ya
Mungu unaotutaka sisi tuunganishwe naye, hawezi kufanya hivyo peke yake.
Anatuhitaji sisi, mapendo yetu ya kumtuliza na ibada zetu ndogo za Malipizi ya
dhambi ili kuziokoa roho motoni. Fumbo la ushirika wa watakatifu limetukuzwa na
ni la kuogopesha, linalofanya wokovu wa roho nyingi kwa kweli utegemee ukarimu
wetu sisi wenyewe! Na ni nia iliyoje ya ukarimu kwa upande wetu! Kwa sababu
tungewezaje kukataa kitendo hiki cha kimisionari ambacho Mama Yetu anategemea
tukifanye, ambacho amekirahisisha sana kukitimiza — kumbuka kwamba kwa ruhusa
ya padri, ibada zote zilizoagizwa zinaweza kuhamishiwa Jumapili — wakati ibada
hizi hizi ni za manufaa sana na zenye kutusaidia sana? Kwani kwa kupitia ibada
hii roho nyingi zilizo karibu sana na hatari ya kupotea milele katika dakika za
mwisho na kama vile ingekuwa licha ya zenyewe, zinaweza kupata neema ya
kuongoka.
Kuutuliza Moyo Safi wa
Maria uliojeruhiwa na miiba, kufanya Malipizi ya dhambi kwa machukizo unayoyapata kutoka kwa wenye dhambi kwa sala na sadaka, hivi ndivyo
lilivyo mwishoni sharti sahihi kuliko yote la hii sehemu ya kwanza ya Siri,
ambayo Mama Yetu alikuja kuikumbusha na kuifafanua Pontevedra mwaka 1925: "Wewe, angalau, jitahidi
kunituliza Mimi." Sasa sadaka kamilifu kuliko zote, sala ya kufaa kuliko
zote, bila shaka ni Sadaka Takatifu ya Misa na Ekaristi Takatifu inayotolewa
kwa Mungu kwa nia ya Malipizi ya dhambi.38
Yote hayo yanatufanya tuelewe kusisitiza kwa nguvu kwa Mama
Yetu, tamaa yake kubwa kwamba ibada hii ya Malipizi ya dhambi ifanywe kila
mahali na mara nyingi kadiri iwezekanavyo. Ibada hii ndiyo inayompendeza kuliko
nyingine yoyote, kwa kuwa ndiyo iliyo kamilifu kuliko zote na kwa hiyo bora
kuliko zote kwa ajili ya wokovu wa roho. Kwa sababu anahitaji ushirikiano wetu
kwa kila namna, ameiwekea ahadi nzuri kuliko zote...
"Vita na amani
vinaitegemea." Kwa kweli, kwa kuongezea wongofu wa wenye dhambi, na
wokovu wetu sisi wenyewe wa milele, Mama Yetu ametaka kwamba Komunio ya
Malipizi ya dhambi iunganishwe na ahadi nyingine kubwa: zawadi ya amani. Tarehe
19 Machi 1939, Sista Lusia aliandika:
"Kuwepo kwa vita au amani ya ulimwengu kunategemea
kutekelezwa kwa ibada hii, pamoja na kujitoa kwa Moyo Safi wa Maria. Ndiyo
maana natamani kusambazwa kwake kwa bidii, hasa kwa sababu huu pia ni utashi wa
Mungu Wetu mwema na wa Mama Yetu mpenzi wa Mbinguni."39
Na tarehe 20 Juni ya mwaka huo huo, aliandika:
"Mama Yetu aliahidi kuondoa balaa la vita, iwapo ibada
hii itasambazwa na kutekelezwa. Tunaona kwamba Atapata kuondolewa kwa adhabu hii
kwa kiasi ambacho juhudi zinafanywa kuisambaza ibada hii; lakini naogopa kuwa
hatujafanya chochote zaidi kuliko tunachokifanya na kwamba Mungu, akiwa
amechukizwa, ataurudisha mkono wa huruma Yake na kuiacha dunia iangamizwe na
adhabu hii ambayo haitafanana na nyingine yoyote iliyowahi kutokea huko nyuma,
ya kutisha, ya kutisha sana."40
Miezi miwili baadaye, vita ilikuwa imekwishatangazwa. Bado
hakuna chochote kilichokuwa kimetekelezwa kulingana na matakwa ya Mbinguni.
"Nataka Kanisa Langu
kuiweka ibada kwa hun Moyo Safi sambamba na ibada kwa Moyo Wangu
Mtakatifu."...Yesu kwa sista Lusia
Kwanza hadi ya Pili
Kutangazwa kwa habari hii ya kiutabiri kunatufikisha sisi
moja kwa moja katika msiba. Ni msiba mkubwa kwa mpigo kidini na kisiasa, ambao
katika muda wa miaka ishirini uliyatumbukiza Ulaya yetu ya Kikristu katika vita
mbaya mno, vita ya mauaji kuliko zote katika historia nzima, na halafu katika
vita nyingine ya umwagaji damu zaidi na ya kutisha katika matokeo yake ya vifo.
Baada ya muda mfupi, uliyatumbikiza mataifa na karibu mabara yote katika utumwa
wa ukatili wa Kirusi. Tutaelezea hivi sasa jinsi Mama Yetu alivyotabiri msiba
huu wa kutisha, tukielezea hatua zake kubwa na vyanzo vya siri tarehe 13 Julai
1917. Hii ni sehemu ya pili ya Siri Yake kubwa.
Siri kuu: Moyo Safi wa Maria,
Wokovu wa Roho. Hata hivyo, hebu tuweke wazi tangu mwanzo kabisa kwamba
hii "siri ya pili" inategemea kwa karibu sana ile ya kwanza, ambayo
ina umuhimu wa kwanza. Kwani kama tutakavyogundua katika sehemu ya pili ya uchunguzi
wetu, mpango mkubwa wa Mungu uliofunuliwa na Malkia wa Mbinguni huko Cova da
Iria, pamoja na ahadi zake za kuvutia za amani ya kudumu ya ulimwengu na pia
vitisho vyake vya adhabu ya kuogopesha — mpango huu mzima wa Mungu ni chombo tu
kinachotumiwa na Huruma ya Mungu kupata wokovu wa roho, wokovu wa idadi kubwa
ya roho kadiri inavyowezekana.
Kwa ujumla, ni lazima turudie katika sehemu ya kwanza ya Siri
kwani bila mashaka yoyote hii ndiyo kuu na ya muhimu kabisa mbele ya macho ya
Mungu. Kuokoa roho, roho zote kutoka kwenye uovu pekee kwa sababu ndiyo iliyo
pekee ya milele, kuziokoa kwa namna yoyote kutoka katika moto wa milele. Hivyo
ndivyo ilivyo pia nia kubwa ya Moyo Safi wa Maria. Pale Fatima aliufunua Moyo
huu Safi kama makimbilio na msaada wa wenye dhambi, hata wale wanaochukiwa na
walio katika hali mbaya kuliko wote, kwa sababu Yeye ni Mpatanishi mwenye
Huruma, na Mlango wa Mbinguni. Hii ni sehemu ya kwanza ya Siri Yake kubwa, kwa
sababu pia ni Siri Yake ya kwanza ya Moyo Wake: Sista Lusia alielezea Siri ya
Kwanza (Maono ya Motoni) katika Kumbukumbu zake (angalia ukurasa wa 17) na
halafu aliendelea kusema:
"Tukiwa tumeogopa sana, na kama vile kwa kuomba msaada, tulinyanyua
macho yetu juu kwa Mama Yetu aliyetuambia kwa huruma na uchungu:
"Mmeiona Jehanamu ambako roho dhaifu za wenye dhambi zinakokwenda.
Ili kuziokoa, Mungu anataka kuanzisha ulimwenguni ibada kwa Moyo Wangu Safi...
..."Kama ninayowaambieni yatatekelezwa, roho nyingi zitaokolewa na
kutakuwa na amani...
"Nitafika kuomba Komunio ya Malipizi ya dhambi kila Jumamosi za
kwanza za mwezi."
Yasinta mdogo alikuwa ameelewa vema onyo hili kubwa la Mama
Yetu kwa wokovu wa roho zetu. Roho yake ilikuwa imepenywa nalo, kama ambavyo
tukio hili la kupendeza linavyoonyesha. "Wakati mwingine, (Sista Lusia
anakumbuka) alikuwa akikusanya maua kutoka shambani huku wakati huo huo akiimba
wimbo aliokuwa ameutunga yeye mwenyewe:
"Moyo Mzuri wa Maria,
ouwe wokovu wangu!
Moyo Safi wa Maria,
waongoe wenye dhambi,
okoa roho zisiende motoni!"
Kwa kweli, maneno haya yanatoa muhtasari wa maana halisi ya
"Siri ya kwanza": Ni kwa kupitia kwa Moyo Safi wa Maria ndiyo Utatu
Mtakatifu unataka leo hii kuokoa roho zetu, roho zote, kuziokoa kutoka moto wa
Jehanamu na kuzifungulia Mbinguni.
Comentários
Postar um comentário